Hotuba ya Katibu wa Taifa la Serikali ya Marekani Hillary Clinton mjini Geneva tarehe 6 mwezi wa kumi na mbili

L’Associazione Radicale Certi Diritti ha tradotto in lingua swahili il testo integrale dell’intervento del Segretario di Stato americano, Hillary Clinton, tenuto il 6 dicembre a Ginevra alla Conferenza internazionale dall’Alto Commissariato delle Nazioni Unite per i Rifugiati in occasione della giornata mondiale dei Diritti Umani alla quale hanno partecipato oltre 145 paesi.

 

Shirika la Radikali Certi Diritti (Haki za Kihakika) limetafsiri matini mazima ya hotuba ya Katibu wa Taifa la Serikali ya Marekani, Hillary Clinton, aliyoinena tarehe sita mwezi wa kumi na mbili mjini Geneva kwenye Kongamano la kimataifa linaloandaliwa na Wizara Kuu ya Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi wa Kisiasa kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ambayo mataifa mia na arobaini na tano yameshiriki.

 

Lo Swahili è una lingua parlata da circa 80 milioni di persone, lingua nazionale in tanzania, kenya e uganda lingua ufficiale dell’Unione Africana. Dialetti swahili sono diffusi dal sud della somalia al nord del monzambico, dal nord del madagascar al sudest della Repubblica democratica del Congo.

il discorso in italiano>
http://www.certidiritti.it/certi-diritti-pubblica-la-traduzione-italiana-integrale-del-discorso-di-hillary-clinton-per-la-giornata-mondiale-dei-diritti-umani

 


Utangulizi    

Shirika la Radikali Certi Diritti (Haki za Kihakika) ni shirika la radikali kwa sababu kinavyotenda kama Chama cha Radikali, yaani linaendelea kupanda kwa lengo kwa lengo na aina ya kupambana kwa kupata malengo yetu ni ile ya Radikali: kutotii kwa kiraia “siyokiugomvi”(aina ya kuandamana bila vurugu na bila kukosea uhuru wa wengine, lakini inaweza kuwa uasi ili tuoneshe tunachotaka); kupendekeza; kuzungumza. Shirika la Certi Diritti linashughulikia haki za kiraia na za kibinadamu hasa uhuru na dhima ya mwelekeo na tabia za kijinsia.  Certi Diritti ni shirika la msingi pamoja na mengine ya Chama cha Radikali. Jina halisi la chama hicho ni PRNTT, yaani Nonviolent Radical Party Transnational and Transparty (Chama cha Radikali Siyokiugomvi Kivukajimataifa na Kivukajivyama). Kwa kweli chama hiki kina katiba ya NGO (Shirika lisilo la kiserikali) na kimo ndani ya “Baraza la Uchumi na Ustawi wa Jamii” (ECOSOC). Kwa habari zaidi uangalie hapa http://www.radicalparty.org/en

Shirika limetafsiri hatuba hiyo kwa sababu linafahamu kwamba haki za binadamu na, kati zao, haki za gay ni jambo la ulimwengu lisilotambua mipaka. Tamaa kwa uhuru na kwa kuheshimiwa haki zetu imo kila mtu popote duniani. Kutotambua haki ni kosa linalosababisha matendo ya uhalifu. Shirika la Certi Diritti baada ya uzoefu nchini Uganda na David Kato Kisule na mtetezi wake ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Heshima wa Shirika, limezidi kushughulikia Afrika. Kutafsiri kwa kiswahili kunamaanisha kutambua kwamba kila utamaduni ni rasilimali ya dunia mzima na hata kwa kupigania haki za binadamu. Kama ipo migogoro kati ya utamaduni na ugay hiyo inatokana na desturi na mila. Desturi na mila zinabadilika daima kutokana na hali ya maisha ya jamii. Popote duniani kuna desturi na mali za kishenzi na zile zilizo njema. Kwa mfano pengine Afrika mashariki zipo desturi na mali za kuwaua maalbino. Je tutaendelea kuwaua kwa sababu huo ni utamaduni ama tunapaswa kuacha desturi hiyo? Kwa hiyo desturi na mila siyo sahihi wakati wote. Jambo hili ni sawasawa kwa suala la ugay.

Serikali au nchi haziwezi kushughulikia kuunganisha maadili na sheria vya dini au tamaduni tofauti, lazima ziwe na sheria zake zenyewe zinazotokana na raia yake. Uhalifu unawezekana kuwa dhambi, hiyo inategemea na dini, lakini katika demokrasia na njia ya maendeleo haiwezekani kwamba dhambi ni uhalifu kama sababu zao zinatokana na dini tu. Kwa uhalifu mtu anapata gereza, hiyo ni sheria ya mtu, kwa dhambi motoni baada ya maisha duniani. Katika demokrasia sababu za sheria zingepaswa kutokana na raia inyochagua watu wanaotawala. Kwa hiyo kutunga sheria inayotangaza kuwa gay ni uhalifu, hiyo ni kuvunja demokrasia, kwa sababu serikali na nchi haziwezi kuamua kwamba kwako tu ni uhalifu, kama zinafanya hivyo zinavunja mkataba na wananchi. Uhalifu ni kukosea mtu, sio kukosea Mungu, kukosea Mungu ni dhambi.

Misingi wa falsafa ya utu (ubuntu, muntu, n.k.), ambayo ni utamadu wa waswahili pia, inayohusu zaidi aina ya kutenda na kuishi duniani (pragmatiki) kuliko falsafa ya nje, inahusu maadili ya mtu na msingi wake ni heshima, uhuru, usawa, amani, ukarimu na kadhalika. Kwa misigi ya falsafa hiyo ingewezekana kujenga jamii mpya yenye makubaliano na ushirikiano kati ya watu wote. Hiyo ni changamoto kubwa, lakini ndiyo ari na nia zetu, kwa matumaini haya, Shirika la Radicakali Certi Diritti (Haki za Kihakika) limefanya kazi hii.

Kielezo cha Tasnifu
Neno la kingereza gay limetumiwa siyo kwa sababu hakuna neno la kiswahili, kwa sababu bado kwa kiswahili maneno kama shoga, msenge, msagaji n.k. yana maana mbaya mno kiasi ambayo watu ambao ni shoga, msenge, msagaji n.k. wanakataa maneno haya. Zaidi maneno mengi ya kiasili kama haya yanaonesha umakini wa waswahili kwa matendo ya kujamii jinsia moja kwa hiyo hatuwezi kusema kwamba mambo haya ni nje ya utamaduni wa swahili, ila inawezekana kusema kwamba yanavunja kakuni ya utamaduni lakini utamaduni kwa ajili ya utajiri wa maneno ya kipekee, yaani kila neno lina maana tofauti, unatambua kwako kwao. Neno la kiswahili shoga ina maana ya mtu anayetenda kama mwanawake kwa hiyo maana yake ni karibu na maana ya transgender, kwa ajili ya maana hiyo gay wengi wanakataa neno hilo na wanaitwa basha au msenge kwa kuonyesha ume wao na kumaanisha kwamba wao wanachukua sehemu ya mwanaume katika uhusiano wa kujamii. Hiyo inatokana na mila na desturi ambazo zinabeba aina ya maisha ya kiasili na aina ya mausiano pia ambayo zinadai kwamba kwa uhusiano wa kujamii lazima uwe na mwanawake na mwanaume, ndiyo maana neno shoga limetumiwa kwa mtu anayeacha kutiwa na uume wa mwengine (basha au msenge). Lakini wapo wengi wanaoacha kutiwa na uume wa wengine na sio shoga, yaani hawaotendi kama wanawake na wanaonekana kama mwanaume kabisa kwa hiyo tunatumia neno gay kwa maana ya kila mtu anayefanya tendo la kujamii jinsia moja, yaani shoga, basha, msenge, msegaji na kadhalika. Neno la kingereza gay sio neno la kiasili kwa kuita shoga, ila katika chimbuko lake ni kilatino na linamaanisha furaha au uchangamfu na baada ya karne kumi na sita waingereza walianza kulitumia kwa maana ya mtu anayevunja maadili, mtu siyo wa kawaida, wakati wa karne ishiri neno gay lilikuwa linatumiwa kwa maana ya kila mtu anayependa kufanya tendo la kujamii jinsia moja. Yalipoanza mapambano kwa haki za gay wao wenyewe walichagua neno gay kwa utambuzi wao na pia kwa kusema g.a.y. ni kifupisho cha good as you (mwema kama wewe).


Hotuba ya Katibu wa Taifa la Serikali ya Marekani  Hillary Clinton mjini Geneva tarehe 6 mwezi wa kumi na mbili.

“Habarini za jioni? Nina adhama na ninapenda sana kuwa hapa. Nataka kuwashukuru Mkurugenzi Tokayev na Bibi Wyden pamoja na mawaziri wengine, mabalozi, weshimiwa na wadau wa Umoja wa Mataifa. Mwishoni mwa wiki hii tutasherekea sikukuu ya haki za binadamu, kumbukumbu mojawapo ya ushindi mkubwa wa karne iliyopita.
Mwaka 1947 wajumbe wa mabara sita walijitolea kuandika Azimio ambalo litatangaze na kudai uhuru na haki za kimsingi za watu wanaoishi kokote duniani. Baada ya Vita Vikuu Vya Pili Vya Dunia, mataifa  yalidai Azimio la aina hii ili lizuie ukatili na lilinde utu na hadhi vilimo kila mtu. Kwa hiyo wajumbe walianzisha kazi hiyo. Walijiadili, waliandika, walisoma, walisoma tena na waliandika tena kwa masaa maelfu. Waliambatanisha ushauri wa serikali, mashirika na wanadamu ulimwenguni  pote.

Saa nane usiku wa tarehe 10 mwezi wa kumi na
mbili mwaka 1948, baada ya takribani miaka miwili ya kazi na usiku wa mwisho wa mjadala, Mkurugenzi wa “Mkutano Mkuu wa UM” alianzisha upigaji kura kuhusu matini ya mwisho. Mataifa arobaini na nane yalikubali, nane yalijihini, hakuna taifa lilikataa: Azimio la Kiulimwengu la Haki za Binadamu lilikubaliwa. Hilo lilitangaza wazo moja ambalo ni la msingi na lenye nguvu sana: wanadamu wote walizaliwa wakiwa huru na sawa katika hadhi na haki zao. Kwa ajili la Azimio hilo imekuwa wazi kwamba haki hazitolewi na serikali, ila anazo kila mtu anapozaliwa.  Suala hili halihusu nchi tunazoishi, nani ni viongozi wetu au hata sisi ni nani. Sote kama wanadamu tuna haki. Kutokana na haki hizi, serikali zinapaswa kuzilinda.

Katika miaka hii sitini na tatu tangu tulipata Azimio hilo, mataifa mengi yamekuza sana haki za binadamu. Polepole mipaka ya zamani –  iliyozuia watu kufaidi uhuru, hadhi na utu vyao halisi – imeanguka. Katika sehemu nyingi sheria za kiubaguzi zimefutwa, desturi za kijamii na kisheria – ambazo kwa ajili yao wanawake walikuwa na hadhi ya tabaka la pili – zimekomeshwa, uwezo wa kundi la watu wachache wa kidini wa kuendelea na dini yao umeidhinishwa.
Matokeo haya hayafiki kirahisi. Watu wengi walipambana, walijiunga na waliandamana kiumma na kibinafsi, siyo kwa kubadilisha sheria tu lakini kwa ufahamu pia. Kwa ajili ya kazi ya vizazi, kwa ajili ya watu maelfu – ambao maisha yao yaliathiriwa na udhalimu – sasa inawezekana kuishi kwa uhuru na kushiriki maisha ya siasa, uchumi na jamii katika jumuiya yao.

Kama sote tunajua kwamba bado kuna mambo mengi ya kufanya ili tuhakikishe  ahadi ile, uhalisia ule na maendeleo yale kwa wote. Leo nataka kuzungumza kuhusu kazi tunayopaswa kuifanya ili tulinde kundi moja la watu ambao haki zao bado zimenyimwa katika sehemu nyingi. Wao ni kundi lisiloonekana. Wanafungwa jela, wanapigwa, wanatishiwa sana na hata wanahukumiwa kifo. Wengi walitendwa kwa dharau na walifanyiwa ugomvi na wananchi wengine huku mamlaka ambazo zilitakiwa kuwalinda ziliendelea, au zilizidi, kuwatenda vibaya zaidi. Nafasi zao za kazi au elimu zimekataliwa, kwa hiyo wanalazimishwa kuacha nyumba zao na nchi zao kujificha au kukataa wao ni nani, kujikataa, ili wajilinde.

Nazungumza kuhusu watu ambao ni gay, lesbian, bisexual na transgender (LGBT), yaani wanadamu  wanaozaliwa huru na wenye usawa na hadhi sawasawa na wengine, watu walio na haki ya kudai. Hiyo ni changamoto inayobaki leo ili tukuze haki za binadamu wote. Nazungumza hivi lakini najua kwamba hata nchi yangu ipo mbali sana kufika ukamilifu juu ya haki za binadamu kwa wana-LGBT. Mpaka mwaka 2003 kuwa gay kulikuwa bado uhalifu katika mataifa mengi. Wamerikani wengi ambao ni wana-LGBT wametendwa kwa ugomvi na kuchokozwa katika maisha yao na wengine, kati yao wavulana na wasichana wengi, wanaudhiwa na watengwa. Hayo yamekuwa mazoefu ya kawaida kwao. Kwa hiyo lazima tufanye kazi sana ili tulinde haki za binadamu nchini kwetu, na popote.

Najua vizuri kwamba suala hilo linavutia wengi na yapo matatizo mengi katika kulinda haki za binadamu kwa wana-LGBT yanayotokana na imani za watu binafsi, siasa, tamaduni na dini. Kwa hiyo nakuja hapa kwa heshima, ufahamu na upole. Hata kama maendeleo ya suala hili siyo rahisi, lazima tushughulikie mapema.  Kwa ajili ya fahamu nataka kuzungumza  juu ya masuala magumu na muhimu tunayoyapaswa kushughulikia sisi pamoja ili tufike makubaliano ya kiulimwengu kuhusu haki za binadamu kwa wana-LGBT popote wanapoishi.

Suala la kwanza ni kitovu cha tatizo. Wengine wanadai kwamba haki za binadamu na haki za wana-LGBT ni tofauti, lakini kwa kweli ni jambo moja. Bila shaka miaka sitini iliyopita serikali zilizoandika na kukubaliana juu ya Azimio la Kiulimwengu la Haki za Binadamu hazikuwaza kwamba kazi hiyo ingehusu haki ya kundi la LGBT. Hata hazikuwaza kama zinahusu wazawa, watoto, waelemavu au makundi mengine yanayobaguliwa. Lakini, katika miaka sitini hii tumetambua kwamba watu wa makundi haya wana haki na hadhi kamili, kwa sababu, kama watu wengine, wana utu.
Ufahamu huo haukufika mara moja au ghafla, lakini polepole. Katika muda huu tumeelewa kwamba kazi zetu ni kuhakikisha kwamba watu wana haki tangu wanapozaliwa, badala ya kubuni haki mpya au za kipekee kwao. Kama kuwa mwanawake, mtu wa kundi la watu wachache la ukoo, kidini au kikabila, kuwa mwana-LGBT haimaanishi sio binadamu. Kwa hiyo haki za wana-LGBT ni haki za binadamu na haki za binadamu ni haki za wana-LGBT.

Ni uvunjaji wa haki za binadamu tunapowapiga au tunapowaua watu kwa sababu ya mwelekeo wao wa kijinsia au kwa sababu wao sio watu wa kawaida kufuatana na mila na desturi juu ya jinsi wanaume na wanawake wanapaswa kuonekana ama kutenda. Ni uvunjaji wa haki za binadamu serikali zinapotunga sheria zinazotangaza wana-LGBT ni wahalifu au wanapoacha kuwaadhibu watu wanaowakosea wana-LGBT. Ni uvunjaji wa haki za bindamu wasagaji au mashoga “wanapoobakwa ili kurekebishwa” au wanapolazimishwa kutumia homoni za kuwabadilishwa au wanapokufa kwa sababu ya uchochezi wa kupigwa au wana-LGBT wanapolazimishwa kukimbilia nchi nyingine ili kulinda maisha yao. Ni uvunjaji wa haki za binadamu tunapobagua au tunapowatenga watu kwa mwelekeo wao wa kijinsia ili wapate tiba, tunapoondosha haki au uhuru vyao vya kutembea barabarani. Siyo muhimu sura zetu, tunatoka wapi, sisi ni nani, bali sisi kama watu tuna haki za binadamu na hadhi yetu.

Suala la pili linahusu asili ya ugay. Wengine wanafikiri kwamba ugay ni jambo linalotoka magharibi, kwa hiyo inawezekana kuukataa nje ya magharibi. Kwa kweli watu walio gay wanazaliwa na wanahusu kila jamii duniani. Wao wana umri wowote, rangi na asili zozote; ni madaktari na walimu, washamba na wanaofanya kazi ya benki, askari na wachezaji; tukifahamu au tusipofahamu, tukitambua au tusipotambua, wao ni familia yetu, rafiki zetu, na majirani zetu.
Kuwa gay siyo uvumbuzi wa magharibi; ni uhalisia wa utu. Kulinda haki za binadamu kwa wote, walio gay na wasio gay, hazifanyi serikali za kimagharibi tu. Katiba ya Afrika Kusini, imeandikwa baada ya Apartheid, inalinda usawa wa wananchi wote, hata walio gay. Nchini Kolombia na Argentina hata haki za gay zinalindwa. Nchini Nepal Korti ya Katiba imetangaza kwamba wana-LGBT lazima wawe na haki sawasawa na watu wengine wote. Serikali ya Mongolia inashughulikia kutoa sheria inayohusu haki za gay.

Sasa, wengi wanafikiri kwamba kulinda haki za binadamu za kundi la LGBT ni anasa wanayoweza kushughulikia mataifa matajiri tu, ila kwa kweli, katika mataifa yote, kutolinda haki hizi kunasababisha vifo vya watu gay na wasio gay kwa sababu ya magonjwa na ugomvi, kunyamazisha sauti na mawazo visivyokubaliwa kusababisha kudumaza jamii, kutofikisha fikra kuhalisiwa na wekezaji walio gay inamaanisha kufuta utajiri. Twalipa gharama hizi kila mara kundi linapotendewa vibaya kuliko mengine. Rais aliyepita wa Botswana, Mogae, katika siku hizi alisema kwamba kama wana-LGBT wanafichwa, haiwezekani kupata mipango kamili ya kupunguza UKIMWI. Hiyo ni kweli hata kwa changamoto nyingine.

Suala la tatu na labda gumu kuliko mengine linahusu sababu za kidini na kitamaduni zinazotumiwa kuvunja au kutolinda haki za binadamu za wana-LGBT. Sababu hizi siyo tofauti sana na sababu zinazotumiwa kutetea matendo ya ugomvi ambayo wanatendwa wanawake kama uuaji wa hadhi, uchomwaji moto wa wajane na ukeketaji wa wanawake. Wengi wanaendelea kulinda matendo haya kwa sababu yanahusu desturi na mila. Lakini unyanyasaji wa wanawake sio utamaduni, ni uhalifu. Sawasawa na utumwa, ambao ulitetewa kama uamuzi wa Mungu na sasa ni ukiukaji wa haki za binadamu.
Katika kila moja ya mambo haya, tumejifunza kwamba hakuna desturi au mila ni muhimu kuliko haki za binadamu tulizonazo sote. Na haya ni kweli hata kwa ugomvi kwa wana-LGBT, kuhukumu hali ama tabia zao, kuwafukuza kutoka katika familia au jamii zao, ama kimyakimya ama kwa uwazi kukubali mauaji yao.

Bila shaka desturi na mila na mafundisho vya kidini au kitamaduni mara chache vinatofautisha sana na ulinzi wa haki za binadamu.  Dini yetu na utamaduni wetu ni chanzo cha huruma na msukumo kwa wanadamu k
ama sisi sote. Hata waliohalalisha utumwa walijitetea kwa dini, pia waliotaka kufuta utumwa walijitetea kwa dini. Tukumbuke kwamba ahadi yetu ya kulinda uhuru wa dini na hadhi za wana-LGBT ina chimbuko moja. Kwa wengi kati yetu imani na mazoefu vya dini ni rasilimali yamaana na fahamu na msingi wa kuwako kwetu kama watu. Sawasawa, kwa wengi kati yetu, mahusiano ya mapenzi na familia ambayo tumeyatengeneza ni rasilimali muhimu kwa maana na utambulisho. Kujali wengine ni kielezo cha kuwa binadamu kamili. Hiyo ni kwa sababu kwako kwa utu ni jambo la kiulimwengu na haki za binadamu la kiulimwengu pia na zinavuka dini na tamaduni vyote.

Suala la nne ni mafundisho ya historia kuhusu namna ya kuelekea kukuza haki kwa wote. Maendeleo yanaanzishwa kwa mazungumzo ya ukweli. Wapo watu wanaosema na wanaofikiri kwamba gay wote ni pedofili, kwamba ugay ni ugonjwa unaoweza kuambukizwa na kutibika, au watu walio gay wanasababisha watu wengine kuwa gay. Dhana hii siyo kweli kabisa. Kuna uwezekano wa dhana hii kutokupotea kama wale wanayoikuza au kukubaliana nayo wanaachiwa badala ya kukaribishwa kushiriki na kuelezea hofu na mashaka yao. Hakuna mtu aliwahi kuacha imani yake kwa sababu alilazimisha kufanya hiyo.
Haki za kiulimwengu za binadamu zinahusu uhuru wa kujieleza na wakuamini, hata kama maneno yetu au imani zetu zinakebehi utu wa wengine. Lakini, hata kama sote tuna uhuru wa kuamini chochote, hatuwezi kufanya kila kitu tunachotaka huku tunapolinda haki za wanadamu wote.

Kufikia ufahamu wa mambo haya unahitaji zaidi ya hotuba. Inahitaji mazungumzo. Zaidi, inahitaji mazungumzo mengi sana katika sehemu ndogo na kubwa. Na inahitaji hiari wa kutambua utofauti kama msukumo wa mazungumzo, na siyo ya kutozungumza.
Lakini maendeleo yanatokana na mabadiliko ya sheria. Katika sehemu nyingi, hata nchini mwangu, makubaliano ya haki yametokea baada ya, sio kabla ya, ulinzi wa kisheria. Sheria inafundisha. Sheria zinazobagua zinafundisha ubaguzi. Sheria zinazotangaza ulinzi wa usawa zinafundisha umuhimu wa maadili ya usawa. Mara nyingi sheria zinapaswa kubadilika kabla ya hofu ya mabadiliko yameachwa.
Wengi nchini mwangu walifikiri kwamba Rais Truman alikosea sana alipoamuru kufuta sheria ya ubaguzi wa rangi katika majeshi yetu. Walidai kwamba hiyo ingaliharibu umoja wa majeshi. Na baada ya uamuzi huo tuligundua kwamba badiliko hilo linaungisha jamii kwa namna ambayo hata wafuasi hawakuwaza. Hivyo  hivyo, wengine katika nchi yangu walidai kwamba mwisho wa “Don’t Ask, Don’t Tell” ungesababisha matokeo mabaya sana kati ya majeshi. Leo, kiongozi wa Marines aliyefikiri hivyo, sasa anasema kwamba alikuwa na hofu bure kwa sababu matokeo yamekuwa mazuri.
Mwishoni, maendeleo yanatokana na hiari ya kutembea umbali ni kujua wengine wanaishi vipi. Tungepaswa kujiuliza: “Ningejisikiaje kama ingekuwa uhalifu kupenda mtu ninayempenda? Ningejisikiaje kama ningebaguliwa kwa jambo langu nisiliweza kulibadilisha?”. Changamoto hii inahusu kila mtu kati yetu, tunapofikiri kuhusu misimamo ya msingi, tunapofanya kazi ili tuvumilie na tuheshimu hadhi za wote, na tunapowasiliana kwa upole na wao hatuokubaliani nao kwa ya matumaini ya kuongeza ufahamu kati yetu.

Suala la tano na la mwisho linahusu kazi tunayoweza kufanya ili wote duniani wakubali haki za binadamu kwa wote, hata kwa wana-LGBT. Ndiyo, wana-LGBT lazima wasaidie kazi hii, kama wengi wenu mlivyoanza kushughulikia. Ujuzi na uzoefu wao ni muhimu sana na ujasiri wao ni changamoto. Tunafahamu majina ya mashujaa wa masuala ya LGBT ambao wametoa maisha yao kwa changamoto hiyo na wapo wengi ambao majina yao hatutayafahamu. Lakini mara nyingi wao ambao haki zao zimekataliwa wamewezeshwa kidogo kuleta mabadiliko wanayoyataka. Wakishughulikia peke yao, hawawezi kupata idadi ya watu wengi wanaoweza kuleta mabadiliko ya kisiasa.
Inapobaguliwa sehemu ya utu, tuliobakia hatuwezi kukaa pembeni. Kila mara mpaka unapofutwa, hiyo inasababishwa na ari waliyoifanya pamoja wao wanaokaa pande mbili tofauti ya mpaka. Katika mapambano ya haki za wanawake msaada wa wanaume ulikuwa muhimu sana. Pambano kwa usawa wa kimbari lilitegemea watu wa kila rangi. Kupambana na ubaguzi wa dini ni kazi ya watu wa kila dini. Hiyo ni sawasawa kwa mapambano ya usawa.

Kinyume, tunapoona ukiukaji au hatia vya haki za binadamu na tusipojali, tunatuma ujumbe kwamba matendo hayo hayasababishi madhara na tunaendeleza hatia na ukiukaji. Lakini tunapotenda, tunatumia ujumbe wenye nguvu ya kimaadili. Hapa Geneva, jamii ya kimataifa imetenda ili kukuza ukubalifu wa kiulimwengu juu ya haki za binadamu za wana-LGBT. Mwezi wa tatu, Ustawi wa Haki za Binadamu, mataifa themanini na matano yalitangaza azimio liliondea kinyume na uhalifu kwa gay na ugomvi unaosababishwa na mwelekeo wa kijinsia na jinsia.

Mkutano wa Ustawi wa Haki za Binadamu mwezi wa sita, nchini Afrika Kusini ilianzisha ilani kuhusu ugomvi kwa wana-LGBT. Wajumbe wa Afrika Kusini walitoa kwa ufasaha hatuba kuhusu uzoefu wao na upiginiaji wa usawa wa utu na umoja wao. Ilipokubaliwa ilikuwa ilani ya kwanza ya Umoja wa Mataifa iliyotambua haki za binadamu za watu walio gay popote duniani. Katika Shirika la Mataifa la Amerika mwaka huu, Tume ya mataifa ya Amerika juu ya Haki za Binadamu ilianzisha kundi linaloshughulikia haki za LGBT, hiyo ni hatua ambayo inaleta matumaini zaidi.
Sasa, tunapaswa kupita mipaka na kufanya kazi hapa na duniani kote ili tuhamasishe watu washughulikie haki za binadamu za kundi la LGBT. Naomba viongozi wa mataifa ambayo watu wanafungwa jela, wanapigwa au wanahukumiwa kifo kwa sababu ya kuwa gay, wawaze hili: maana uongozi ni kuwa kichwa cha raia inapohitaji. Inamaanisha kulinda hadhi ya wananchi wote na kuchochea wengine kutenda hivyohivyo. Inamaanisha pia kuhakikisha kwamba wananchi wote wanatendewa kwa usawa kwa sheria ya taifa, na sisemi kwamba gay sio wahalifu. Wanavunja sheria kama wale wasio gay. Wanapofanya hivyo lazima wahukumiwe, lakini kuwa gay sio uhalifu.

Nawambia raia wa kila taifa kwamba kujali haki za binadamu ni kazi yenu. Maisha ya gay yanategemea sheria lakini pia na matendo wanayotendewa kila siku na familia na majirani zao. Eleanor Roosevelt, aliyechangia ukuaji wa haki za binadamu duniani, alisema kwamba haki hizi zinaota katika sehemu iliyo karibu nyumbani – barabarani wanapoishi watu, shuleni wanaposoma, viwandani, mashambani na ofisini wanapofanya kazi. Sehemu hizi ni uwanja wenu wa kutenda. Matendo mtakayoyaanzisha na mawazo mtakayoyadai yatasababisha uotaji wa haki za binadamu pale mnapoishi.
Mwisho, kwa wana-LGBT wa dunia, waniache niseme hivi: popote mnapoishi na kwenye hali yoyote ya maisha, kama mnapata msaada au mkijisikia kubaguliwa na wanyonge, jueni hampo peke yenu. Wapo watu kila mahali duniani wanaofanya kazi kwa nguvu ili kuwasaidieni kuondosha dhuluma na hatari mnayoivumilia. Hiyo ni kweli kwa nchi yangu: Marekani ni msaidizi wenu na merekani ni rafiki zenu.
Utawala wa Obama unalinda haki za binadamu za wana-LGBT kama sehemu ya siasa yetu juu ya haki za binadamu na ni kipaumbele cha sera ya nje. Katika ubalozi wetu mabalozi wanaanza kuleta changamoto juu ya kesi maalum na sheria na wanafanya kazi na wadau wanaokuza ulinzi wa haki za binadamu  kwa wote. Jijini Washington tumeanzisha ‘task force’ katika Wizara ya Taifa ili kusaidia na kupanga kazi hiyo. Tumeanzisha pia mpango wa msaada wa dharura wa ulinzi wa haki za binadamu walio LGBT.

Asubuhi hii jijini Washington, Rais Obama alianzisha mkakati wa kwanza wa kiserikali kwa kupambana na ukiukaji wa haki za binadamu za wana-LGBT nje ya Marekani. Akijenga juu ya mikakati iliyoanzishwa na Wizara ya Taifa na serikali mzima na Rais ameamuria mashirika ya serikali yanayokaa nje ya Marekani yapambane na ukiukwaji wa haki dhidi ya wana-LGBT, kuzidi kulinda wakimbizi wa kisiasa wa LGBT, kuhakikisha msaada wetu wa nje ili kuzidisha ulinzi wa haki za LGBT, kuhusisha mashirika ya kimataifa kwa mapambano dhidi ya ubaguzi na kuanzisha mipango ili tukatae ugomvi kwa LGBT.

Nafurahi kutoa taarifa kwamba tunaanzisha Mfuko wa Kimataifa wa Usawa unaosaidia kazi za mashirika ya raia wanaoshughulikia m
ambo haya popote duniani. Mfuko huu utayasaidia kupanga vizuri matendo, kujifunza kutumia sheria kama chombo kinachowasaidia, kutumia vizuri fedha zao, kufundisha washirika wao, na kuanza kushirikiana na mashirika ya wanawake na makundi mengine yanayoshughulikia haki za binadamu. Tumepanga zaidi ya milioni tatu ya dola za kimarekani kwa ajili ya kuanzisha Mfuko huo na tunatumaini wengine watachangia fedha.

Wanawake na wanaume wanaopambana kwa ajili ya haki za binadamu kwa wana-LGBT katika sehemu ambayo ni hatari sana, wengine kati yao wapo hapa leo, wao ni hodari na wanastahili msaada wetu wote tunaoweza kuwapa. Tunajua hiyo ni changamoto nzito, bado tunapaswa kufanya kazi sana, lakini wengi kati yetu waliona mambo yanaweza kubadilika haraka. Wakati wa maisha yetu, tabia ya watu kwa gay katika sehemu nyingi imebadilika. Wengi, mimi pia, katika miaka hii wameimarisha msimamo wao kuhusu eneo hili na tumeanza kujali zaidi, kuzungumza, kushiriki na kuanzisha mahusiano ya kibinafsi na kikazi na watu gay.

Maendeleo haya yanaonekana sana katika sehemu nyingi. Tuchukue kama mfano wa Mahakama Kuu ya Dheli iliyoamua miaka miwili iliyopita kwamba kuwa gay nchini Uhindi siyo kinyume cha sheria, nataja: “kama ipo kanuni muhimu kwenye Katiba ya Uhindi ni ushirikishwaji”. Sina shaka ushirikiano kwa haki za binadamu kwa LGBT utaendelea kukua. Kwa sababu ya maoni ya vijana wengi hili limekuwa jambo rahisi: watu wote  wanastahili kutendewa kwa heshima na kuheshimu haki za binadamu na kwa hiyo siyo muhimu nani wanaowapenda.

Ipo sentensi tunayoitumia tunapohamasisha wengine kushiriki katika haki za binadamu: “Ukae upande sawa wa historia”. Historia ya Marekani ni historia ya taifa inayohusu mapambano mengi dhidi ya ubaguzi na kutokuwa usawa. Tulipambana vita kali ya kiraia dhidi ya utumwa. Katika nchi mzima watu maelfu walijiunga kutambua haki za wanawake, za wazawa, za watu wachache wa ukoo, za watoto, za walemavu, wahamiaji, wafanya kazi na kadhalika. Safari inayoelekea usawa na haki inaendelea. Wanaopambana kwa ajili ya haki za binadamu walikaa na wanakaa upande sawa wa historia na historia inawaheshimu. Waliojaribu kuharibu haki za binadamu walikosa na historia inaonesha hilo.

Najua kwamba mawazo niliyowashirikisha leo yanahusu masuala juu ya misimamo inayoendelea kubadilika. Kama inavyotukia mara nyingi, misimamo mingi inayoelekea ukweli, itafika, ukweli ule hauwezi kubadilishwa yaani watu wote walizaliwa wenye uhuru na hadhi na haki sawa. Tumeitwa tena kuhakikisha maneno ya Azimio la Kiuliwengu la Haki za Binadamu. Tujibu wito huu. Tukae upande sawa wa historia, kwa raia wetu, kwa nchi zetu, kwa kizazi kijacho, maisha yao yanategemeana na matendo yetu leo. Nazungumza kwa matumaini sana na naamini hata kama njia bado ni ndefu, tutaendelea pamoja kwa ufanisi. Asante sana.”

 

È la prima volta che passi di qua?

Siamo un’associazione che si occupa di libertà sessuali, fuori da ghetti e stereotipi. Non pensiamo di essere una minoranza semplicemente perché ci occupiamo delle libertà di tutti: anche delle tue. Se ti è piaciuto quello che hai letto, torna più spesso: abbiamo tante cose di cui ci occupiamo da raccontarti. Tutte queste cose le facciamo solo grazie a chi ci sostiene. Puoi farlo anche subito.

Dona ora

Vuoi dare una mano?

Iscriviti a Certi Diritti per un anno. Sono 50 euro spesi bene. Per la tua libertà e quella di tutte e tutti. Troppi? Puoi anche donare 5 euro al mese.

Iscriviti

Chi te lo fa fare?

Di darci dei soldi per portare avanti quello che facciamo già adesso senza chiederti nulla? Nessuno: però se nessuno dona o si iscrive per sostenere i costi delle nostre attività, queste attività non si faranno. E saremo tutti un po’ meno liberi e con meno diritti.

Dona ora

Newsletter

Iniziative, appuntamenti…
Rimani in contatto!

Facebook Twitter Instagram Whatsapp